30.4.2017
saat

All Language

Uıslamu Imanı Na Matendo

     Kila mwenye akili timamu anafahamu kuwa ulimwengu huu umeumbwa kwa lengo maalum.ili kutimiza lengo Allah ameituma mitume pamoja na dini ili kuwaongoza watu. Waislamu walipoutekeleza uislamu wao imani zao zilionekana katika matendo waliokuwa wakiyatenda.Ibada zimekuwa zikitekelezwa bila kufikiriwa kanakwamba ni ada na desturi za jamii ya huku roho ya uislamu ikikosekana kabisa.Kitabu hiki kinalenga kuangaza eneo la kiroho la ibada za kiislamu na kuzipamba kwa vazi la na visa vya mitume na vmaswahaba wao na Masuffi wema.


Othman Nuri Topbash
ISBN: 978-9944-83-711-8

  

Kiigizo Kisichokuwa Na Mfano Muhammad Mustafa

     Mwenyezi Mungu mtukufu alimtuma mtume kuwa ni rehma ya milele kwa viumbe wote.Mtume mtukufu ndiye aliyekuwa kielelezo kamili katika kumfunda na kumlea mwanadamu kwa mifano ya kimatendo isiyokuwa na kikomo na ambayo ilishuhudiwa katika maisha yake. Bila shaka hakuna kiigizo kinachofanana nae, na mafanikio ya wanadamu ni katika kumuiga na kumfuata na kujitahidi kufungamana na shakhsia yake ikiwemo kumpenda toka nyoyoni.Mwandishi amefafanua umuhimu wa kumuiga pia ameelezea visa na hali mbalimbali za mtume mtukufu Muhammad Mustafa (s.a.w).


Othman Nuri Topbash
ISBN: 978-9944-83-669-2

  

Pumzi Ya Mwisho

     Kuvuta pumzi ya mwisho ni jambo lisilokwepeka kwetu wanadamu. Swali muhimu kulitengezea majibu kwa wakati huu ni jinsi gani utaivuta? Kwa kila pumzi maisha yetu yanarefuka, lakini siku moja suala hili litasimama. Ustadh Othman Nuri Topbas ametupatia ukumbusho adhimu wa namna ya kujindaa na umauti ndani ya kitabu hiki, wapo walioishi maisha furaha yakeli lakini wakaikosa ladha nzuri ya pumzi hiyo wakatamani kuongezewa japo sekunde chache ili warekebishe hali zao hizo za mwisho na pia wapo walioishi pasi na kujali wala kufahamu umuhimu wa maandalizi ya jambo hili lakini mwisho wa uhai wao wakabadilika, wakaamini na kujikuta wakiivuta pumzi hiyo kati hali ya salama na amani.


Othman Nuri Topbash
ISBN: 978-9944-83-712-5

  

Hadithi 40 Za Watoto Pamoja Na Visa

     Maneno ya mtume (s.a.w) yanaitwa hadithi. Mtume wetu mpendwa alituletea Qur an au maamrisho ya M/mungu. Alitufafanulia maamrisho haya kupitia hadithi zake.Kupitia maneno yake alitufundisha yale tunayohitajika kuyafanya ili tuwe wenye furaha katika maisha haya na kesho akhera.Tunatakiwa kuyasoma mara kwa mara maneno ya mtume s.a.w. Ninafahamu kuwa wengi wanapenda kusoma visa hivyo nami nimekuletea hadithi arobaini sambamba na visa mbalimbali vyenye kutufunza mbao ya dini yetu.


Prof. Dkt. M.Yasar Kandemir
ISBN: 978-9944-83-671-5

  

Ikhilas na Taqwa

     Maisha ya mwanadamu hutumika kwa hali moja au nyingine, jambo muhimu ni jinsi gani yanatumika, aidha yatumike katika uchamungu yawe ya Ikhlas kwake au yatumike katika ujahili na yasiwe na maana yoyote.Taqwa ni kule kuyadhibiti matamanio ya kimwili na kuimarisha nguvu ya kiroho kwa binadamu.Hivyo Taqwa huhitajika katika kila eneo la maisha, katika imani, ibada, mahusiano yetu na wengine na hata katika kila pumzi ya uhai wetu. Mafanikio ni jambo ambalo kila mmoja wetu anahitajia kupata. Allah anasema Kwa hakika amefaulu aliyeitakasa nafsi yake, (Ala, 87:14).


Othman Nuri Topbash
ISBN: 978-9944-83-683-8

  

Siri katika upendo wa Mungu

     Mwenyezi Mungu Mtukufu aliujalia uhai kwa siri pekee: Ameuumba kutokana na upendo. Kwa sababu hiyo, kuna upungufu popote ambapo upendo haupo na kuna alama za ukamilifu popote upendo ulipo. Ndio maana njia pekee kwa binadamu kufikia radhi za Mwenyezi Mungu Mtukufu na uombezi wa Mtume (s.a.w) - na hivyo kupata wokovu katika dunia hii na Akhera - ni ukweli rahisi ulio ndani ya siri ya upendo. mwandishi Othman Nuuri Topbash ameuelezea ukweli huu katika kitabu hiki, wale wenye kuujua ukweli huu wakatii maagizo yake hupata hisia kali katika nyoyo zao, Allah atujaalie miongoni mwa walioujua ukweli huo. Na kuifuata njia iliyonyooka.


Othman Nuri Topbash
ISBN: 978-9944-83-692-0

  

Sımulızı Ya Fılımbı Ya Mwanzı

Othman Nuri Topbash
ISBN: 978-9944-83-667-8

  

Hijjah Mabrur na Umrah

Othman Nuri Topbash
ISBN: 978-9944-83-690-6

  

Uıslamu

Dkt. Murat Kaya
ISBN: 978-9944-83-686-9

  

  1. Page :
  2. |
  3. 1
  4. |
  5. 2
  6. |
  7. 3
STATISTICS :    Total number of languages : 50    Total number of materials : 1.304    Total number of downloads : 746.692      ALL STATISTIC 

Coded by Gümüş Kelebek